Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo,
Amima Simbo alithibitisha vifo vya watu saba waliofikishwa hospitalini
hapo.
Kwa mujibu wa muuguzi huyo, maiti zilizopokelewa
hospitalini hapo zilionekana zikiwa na matundu yanayodhaniwa kuwa ni ya
risasi, baadhi yao kichwani, begani, viunoni na tumboni.
Aidha majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo pia walikuwa na majeraha mbalimbali ikiwamo ya risari.
Habari zaidi zinaeleza kuwa vurugu hizo zilizuka
baada ya kundi la waandamaji, wengi wakiwa vijana waendesha pikipiki
maarufu kama bodaboda waliokuwa wakipinga mwenzao kukamatwa na kutaka
kuvamia Kituo cha Polisi ili kumwokoa.
Vurugu hizo ziliendelea kuutikisa Mkoa wa Mtwara
kwa siku ya pili mfululizo na kuutikisa Mkoa wa Mtwara, baada ya vurugu
nyingine kuibuka wilayani Masasi jana.
Habari zinasema mbali na vifo na majeruhi, nyumba
za wabunge wawili wa wilaya hiyo zimechomwa moto, ambapo pia magari,
trekta, Ofisi za CCM Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya
ziliharibiwa kwa kuchomwa moto.
Wabunge ambao nyumba zao zimemwa moto ni Mariam Kasembe wa Masasi Mjini na Anna Abdallah Mbunge wa Viti Maalumu wilayani humo.
 |
No comments:
Post a Comment