Wednesday, January 23, 2013

CHADEMA WAMESEMA KAULI ILIYOTOLEWA NA NAPE NNAUYE HAINA UKWELI WOWOTE

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimesema kuwa kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, NAPE NNAUYE, kuwa chama hicho kitakufa kutokana na kuwa na Sumu ya Ubaguzi, haina ukweli wowote, na kumtaka kiongozi huyo kutafakari zaidi kauli hiyo kwa maslahi ya Chama chake.
Akizungumzia kauli hiyo Mkurugenzi wa Sera na Mafunzo wa CHADEMA, BENSON KIGAILA, amesema CHADEMA hakiwezi kufa kwa dhana iliyozungumzwa na NAPE, na badala yake Chama hicho Tawala ndicho kinachoweza kufa kutokana na kukabiliwa, na changamoto nyingi ikiwemo ufisadi.
Katika Hatua nyingine CHADEMA kimemtaka Naibu Katibu wa CCM, MWIGULU NCHEMBA, kutoa ushahidi wa kauli aliyoitoa hivi karibuni, kuwa Chama hicho kimekuwa kikipanga mipango ya mauaji na kubanisha kuwa kauli hiyo, imelenga kulidhalilisha jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa

No comments:

Post a Comment