Tuesday, January 15, 2013

Q-Chilla "Hii Ndio Sababu Iliyonifanya Niingie Kwenye Utumiaji Wa Madawa Ya Kulevya..."



Msanii wa kizazi kipya maarufu kama Q Chilla ambae hapo nyuma alitamba sana na baadhi ya ngoma zake kama Ulisema, Si Ulinikataa, Nakupenda, Wiper na ya sasa inayoitwa Butterfly, amesema sababu ya yeye kumfanya atumie madawa ya kulevya ni baadhi ya watu kumrudisha chini na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia.
       Chilla alikataa kuwataja watu hao ambao walikuwa wakifanya kila jambo ili yeye asifanikiwe na kujikuta katika wakati mgumu. Ila Qchief aliongeza kwa kusema kuwa hadi sasa hajui alimkosea nani na nani wa kumuomba msamaha. Hata hivyo alisema anawashukuru watu wa karibu ambao waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kumshauri aache kutumia madawa hayo.
       Pia Q Chilla alisema kuwa anawashauri wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na wajaribu kushika dini. Pia aliipongeza hatua ya Raisi Kikwete ya kumsaidia Ray C ambaye alikuwa ameingia kwenye wimbi hilo na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya wajitokeze ili wasaidiwe na jamii.
       Q Chilla aliongeza kwa kusema kuwa kwasasa anafanya muziki ambao unalenga soko la kimataifa zaidi mfano Psquare na kusema tatizo la wasanii wengi huishia kusikika nchini tuu na kujiwekea mipaka ya kulenga soko la ndani tu na alimalizia kusema kuwa hana mpango wa kutoa album ila ataendelea kutoa ngoma kali.

Source:gongamx.com

No comments:

Post a Comment