Thursday, January 10, 2013

MAPIGANO YA KIKABILA YATOKEA TENA KENYA

Takriban watu 8 wameuwawa katika mapigano ya kikabila Kusini Mashariki mwa Kenya. Hii ni kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini humo
Mauaji hayo yaliofanyika hapo jana katika eneo la Tana River yalitokea wakati kukiwa na takriban wanajeshi 1000 waliopelekwa katika eneo hilo ili kusimamisha mapigano kati ya kabila la Pokomo na Orma.
Kulingana na Caleb Kilunde afisa wa shirika la msalaba mwekundu, watu wawili kati ya wanane waliouwawa wanaaminika kutoka katika kundi la washambuliaji walioanza kuishambulia jamii ya wa Orma katika kijiji cha nduru. Caleb amesema watu wengine watatu walipata majeraha mabaya ya kichwa na kwamba hali mpaka sasa ni ya wasiwasi kwa kuwa harakati za kulipiza kisasi huenda zikawa zinapangwa.

No comments:

Post a Comment