Kesi
inayowahusu wanaume watano wanaoshukiwa kumbaka msichana mmoja mwenye umri wa
miaka 23 na kisha kumuua nchini India itaanza kusikilizwa leo mjini Delhi.
Mshukiwa
wa sita anayemainika kuwa na umri wa miaka 17, anatarajiwa kufikishwa katika
mahakama ya watoto.
Kesi hiyo
iliwashangaza wengi sana nchini India na kuzua mjadala kuhusu jamii
inavyowachukulia wanawake. Wakipatikana na hatia , huenda wakanyongwa.
Wakili wa
mmoja wa washukiwa alisema kuwa anapanga kuiomba mahakama ya juu zaidi
kuhamisha kesi hiyo nje ya mji wa Delhi.
Wakili
huyo, VK Anand, anasema kuwa hamu ya vyombo vya habari kufuatilia kesi hiyo kwa
karibu huenda ikasababisha hukumu isiyo ya haki.
''Tuna
uhakika hatutapata haki katika kesi hii, ikiwa itasikilizwa mjini Delhi,"
alisema.
Mbali na
hayo, mamake mwathiriwa amelaani matamshi ya baadhi ya watu kuwa mwanawe ndiye
alisababisha jambo lililomkumba.
Aliambia
BBC kuwa wanasiasa waliotoa matamshi kama hayo, ni wabaguzi wa kijinsia na vile
vile hawana maadili na kuwa ni baadhi ya wale wanaounga mkono vitendo kama
hivyo.
'Ushahidi wa kina'
Kitendo
cha unyama kilichofanyiwa mwanamke huyo, kimesababisha ghadhabu na maandamano
kote nchini kuhusu jamii inavyowatendea wanawake, India na serikali imesema
kuwa itaweka sheria kali kuhusu dhulma dhidi ya wanawake
Pia
imeahidi kuendesha kwa haraka kesi za ubakaji katika siku za usoni. Baadhi ya
kesi nchini India huchukua miaka mingi kukamilika.
Kitendo
hicho kilizua ghadhabu kote nchini India
Serikali
ilitangaza wiki jana kuwa inaanzisha mahakama sita za kusikiliza kesi kwa
haraka, mjini Deljhi, ili kuhakikisha kesi za uhalifu dhidi ya wanawake
zinasikilizwa kwa haraka.
Wiki jana
wakili mwingine alidai kuwa wanaume hao waliteswa na kulazimishwa kukiri
kufanya kitendo hicho.
Hata
hivyo maafisa walikataa kujibu tuhuma hizo, kwa sababu za kisheria.
Hata
hivyo mawakili wao wamesema kuwa watakana mashtaka, ingawa viongozi wa mashtaka
wanasema wako na ushahidi wa kutosha dhidi yao.
Mwathiriwa
wa kitendo hicho, ambaye alikuwa mwanafunzi na ambaye hawezi kutajwa kwa sababu
za kisheria pamoja na rafiki yake walishambuliwa kwenye basi wakielekea
nyumbani . Alifariki wiki mbili baadaye hospitalini nchini Singapore.
Wanaharakati
wanataka kubuniwa sheria kali dhidi ya wabakaji pamoja na mageuzi katika idara
ya polisi ambao wamelaumiwa kwa kukosa kuwashtaki washukiwa wa uhalifu
No comments:
Post a Comment