Tuesday, January 22, 2013

DHAMANA YA ELIZABETH MICHAEL (LULU) ITASIKILIZWA TAREHE 25 IJUMAA



Ile kesi inayomkabili msanii wa filamu nchini tanzania elizabeth michael (lulu) imeingia hatua nyingine.
Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam,Januari 25 mwaka huu, itasikiliza ombi la kupatiwa dhamana msanii wa Filamu nchini, Elizabeth Michael (Lulu) ambaye anakabiliwa na kesi yenye namba 125/2012 ya kumuuwa bila kukusudia msainii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Ombi hilo la dhamana ambalo tayari limeishapangiwa Jaji Zainabu Mruke kuanza kulisikiliza ombi hilo wakati bado kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia bado haijapangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa, limewasilishwa mahakamani hapo na mawakili wa Lulu ambaye anaishi gereza la Segerea .
Mawakili hao ni pamoja na Peter Kibatara,Kenned Fungamtama ,Fulgence Massawe,mawakili hao wa Lulu wamewasilisha ombi lao chini ya kifungu cha 148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .

“Lulu ni mtu maarufu nchini, anaiomba mahakama hii impatie dhamana na yupo tayari kutimiza masharti ya dhamana yatakayo tajwa na mahakama hii, na anaahidi kuyatimiza masharti hayo wakati akisubiri kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia itakapopangiwa tarehe

Source:The Super Stars

No comments:

Post a Comment