Monday, January 14, 2013

PRESS RELEASE UTABIRI 2013



Ndugu wanahabari wa vyombo vyote vya habari hapa nchini

Assalaam Aleykum,

UTANGULIZI:

Tarehe kama ya leo, mwaka 2012 ambayo ilikuwa siku ya Ijumaa nilikuiteni hapa kuzungumzia Utabiri wa mwaka 2012 ambao kinyota bado unaendelea. Utabiri huo utakoma Machi 20, Mwaka huu 2013 kwa maana tarehe 21 Marchi ndio mwaka mpya wa kinyota na ambapo ndipo Utabiri rasmi wa mwaka 2013 utakapoanza.

Wengi wenu mmeona na Ni imani yangu na yetu kwamba asilimia 95 ya Utabiri tulioutabiri Januari 13 mwaka 2012 umefanikiwa na yaliyotabiriwa yametokea kama tulivyouweka hadharani. (Nakala ya Utabiri huo nimeambatanisha)

Bila kujisifu, hali hii inaoonesha wazi kuwa Muasisi wa kazi hizi katika Afrika ya Mashariki na Kati na Dunia nzima kwa ujumla, Sheikh Yahya Hussein ambaye kwa sasa ni Marehemu, alirithisha kazi zake hizi kwa mtu Jadidi, Mweledi na Makini kama alivyokuwa akimuomba Mwenyezi Mungu siku zote katika uhai wake.

Kabla sijatangaza rasmi Utabiri wa Mwaka huu, kwanza kabisa nitazungumzia namna mwaka 2013 ulivyoingia.

Mwaka wa 2013 umeanzia siku yaJumanne, siku hii inatawaliwa
Na Sayari ya Mars au Mariikh ambayo nyota zake ni mbili nazo ni nyota ya Punda au Aries na Nge ambayo ni Scorpio

Kinyota hii nyota ya Punda ni nyota ya mwanzo ambayo ndio kichwa na kama nyumba ya Mwanzo na maana yake ni Mwanzo wa jambo, Anza jambo,Tangaza jambo au kupata mafanikio.

Nyota ya Pili ni NGE au Scorpio ambayo Kinyota ni nyota ya Nane au Nyumba ya Nane, nyota hi iinaashiria, Hasira, kupotea, Kuachana, kukimbiwa, Maziko,Vifo na Wasiwasi

Kwa kawaida Mwaka ukianzia siku ya Jumanne unaashiria Matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na kuongezeka Vita sehemu mbali mbali za dunia, Viongozi wa kidini, kisiasa, na kijamii kuugua sana na wengine kufa, kutokea moto katika miji mikubwa, ukame, ukosefu wa Maadili, wafanyakazi kuwapiga mabosi wao, uongo kuwa mwingi kwa maana propaganda, umbeya, masengenyo, mashujaa kufariki, mazao kupungua, ajali kuwa nyingi za bara na baharini na angani, watu kuwa na khofu na watu wengi kuuwawa

Kwa upande mwingine inaashiria biashara kuongezeka na neema kuwa kubwa na watu kufaidika katika biashara

Pamoja na hayo kutakuwa na Matatizo ya maradhi kwa watoto hasa kuugua vifua na maradhi ya kichwa, wanawake wajawazito kupoteza maisha kwa wingi au kuzaa kwa matatizo makubwa

Kwa upande wa Siasa Mwaka ukianzia siku ya Jumanne basi hutokea kwamba Viongozi wa Kidini na kisiasa kutoa matamshi ya utatanishi na kusababisha khofu kubwa na hata watu kupigana lakini hali hiyo hudumu kwa muda mfupi, baadhi ya viongozi hukaa pamoja na kukubaliana mambo baina yao na kurejesha hali ya utulivu na amani

Mwaka huu wa 2013 Mwezi utapatwa mara tatu tarehe 25/4/2013 ambayo itakuwa siku ya Alkhamisi, tarehe 25/5/2013 ambayo itakuwa siku ya Jumapili na tarehe 18/10/2013 siku ya Ijumaa
Jua lenyewe nalo lipatwa mara mbili tarehe 10/5/2013 ambayo itakuwa siku ya siku ya IJumaa na tarehe 3/11/2013 itakuwa siku ya jumapili
Siku hizi za Alkhamisi Ijumaa na Jumapili ambazo Jua na Mwezi utapatwa zina athari ya moja kwa moja kwa maisha yetu, Alkhamisi inatawaliwa na Sayari ya Jupite r ambayo inahusika na Serikali, Wizara. Safari, na Magomvi,
Siku ya Ijumaa inatawaliwa na Sayari ya Venus au Zuhura ambayo inahusika na Muafaka, Urafiki,, Mapenzi, Ndoa, Masikilizano, Mapatano, Mambo ya Muziki, Wasanii, na Michezo.
Siku ya Jumapili inatawaliwa na Sayari ya Jua ambayo inahusika na Kiburi, Nguvu, Ufahari, Kuona haya, wanasiasa, madereva, mafundi wa mambo ya moto na magari.
Huu Mwaka wenyewe 2013 namba mbili za mwisho 13 ukizijumlisha unapata 4 ambayo ni nyota ya Kaa au Cancer ambayo inahusikana ,Kilimo, Mapenzi, Unyonge, Kufanya vitu kwa vishindo, Siri na kuvumbuka kwake, Kuvunjika biashara na kutimia kwa haja, Mvua na Mafuriko na Majanga ya asili.
KUTOKANA NA HAYO MAELEZO:-
Hali ya Kijamii:

Natabiri: kwamba katika Mwaka huu wa 2013 Ndoa nyingi zitavunjika. Watu wengi, wakiwemo Mawaziri na Viongozi Waandamizi wake kwa waume, watajikuta katika kashfa ya Ngono, Kufumaniwa au kufumania na kupigana kiasi cha baadhi yao kuuawa.

Natabiri; Kuwa maisha katika mwaka huu yatakuwa mazuri, lakini kwa Watanzania watakaojifunga mikanda kuelekea katikati ya mwaka 2013.

Natabiri: Maradhi ya watoto kuongezeka katika Mwaka huu wa 2013 na hasa ya kifua na kichwa. Wanawake wengi wajawazito watapoteza maisha kwa kujifungua na au kuzaa kwa matatizo makubwa ambayo hayajawahi kuonekana.

Natabiri: Ajali zitakuwa nyingi, kuchafuka kwa bahari kutakuwako kwa wingi na kutakuwa na hofu ya watu wengi kuuawa.

Natabiri: Kutokea kwa mioto mikubwa kwenye miji mikubwa, Njaa kuongezeka, ukosefu wa maadili, wafanyakazi kuwapiga mabosi wao, uongo mwingi kwa maana ya propaganda,

Natabiri: Umbeya utakua kwa kiwango kikubwa mwaka huu wa 2013, pamoja na masengenyo.

Natabiri vifo vya Mashujaa au wale watakojiona ni mashujaa.

Natabiri: wingu zito la vifo vya ghafla kwa watunzi wa hadithi na vitabu, Waandishi wa habari, Wanasiasa na Wasanii na muda huu itakuwa mbaya zaidi ya mwaka jana.
Hali ya Kisiasa:

Natabiri: Viongozi wengi wakiwemo Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wenyeviti wa vyama na Makatibu wao watatoa matamshi ya utatanishi na kusababisha khofu na mitafaruku mikubwa itakayowafanya watu kupigana.

Hata hivyo, hali hiyo itadumu kwa muda mfupi. Kwani baadhi ya viongozi watalazimika kukaa pamoja na kukubaliana mambo baina yao na kurejesha hali ya utulivu na amani.

Natabiri: Wabunge wengi katika Bunge la Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania wataungana katika masuala yatakayohusu Utaifa bila kujali itikadi zao za kivyama au kimajimbo. Hata hivyo, nyota zinaonesdha kuna baadhi ya wabunge wataanguka Bungeni wakati wa majadiliano.
Kinyota haionekani kuwa kutakuwa na athari lakini itapaswa kufanyika juhudi za ziada kuokoa maisha yao.
Natabiri Rais Jakaya Kikwete maarufu kama “JK” kufanya mambo ya ajabu na yasiyotabirika na ataungwa mkono kwa asilimia 100 na wananchi wote wa Bara na Visiwani.

Natabiri JK atatenda maamuzi magumu katika mwaka 2013 kiasi cha dunia kushangaa.

Natabiri: JK ataendelea kupata wasaidizi sadifu hasa kwa upande wa Uwaziri. Vile vile nyota za Mawaziri Harrison Mwakyembe, John Pombe Magufuli na Khamisi Kagasheki zitazidi kungara Mwaka huu na kuungwa Mkono na Wananchi

Natabiri JK ataunganisha nchi na kuwa moja yenye uimara wa Utaifa kuliko watangulizi wake. na atashirikiana zaidi na Wanasiasa na viongozi wa dini kuondoa mtikisiko wa uvunjifu wa amani uliokuwapo nchini mwaka jana.
Natabiri Chama kimoja cha siasa hapa nchini kuchochea kujitenga na kuunda Taifa lake. Hata hivyo, kusudio hilo halitafanikiwa. Kwani litapingwa na Watanzania wote kwa kauli na vitendo.

Natabiri:. Tanzania kushinda kwa kishindo kwenye mgogoro wake na Malawi kuhusu Ziwa Nyasa bila kupigana vita.
Hali ya Kibiashara

Natabiri: Mauzo ya bidhaa yataongezeka na kuongeza neema na watu kufaidika katika biashara. Pia mwisho wa mwaka huu wa 2013 mvua zitaongezeka na mazao yatakuwa mengi.
Natabiri: Wafanyabiashara wengi na hasa wajasiriamali kufanikiwa katika kazi zao.
Natabiri: Neema itawaangukia wajasiriamali wa aina zote hapa nchini kwa mwaka huu.

Natabiri wawekezaji wengi zaidi mwaka huu watajikita kwenye biashara ndogondogo kuliko ilivyokuwa katika miaka iliyopita.

Natabiri: Sakata la gesi ya Mtwara litatulia na kumalizika kwa amani katika mwaka huu wa 2013 kwa wananchi wote kuungana na kuunga mkono matumizi yake kwa faida zaidi ya Taifa badala ya jimbo au majimbo

Natabiri: Nchini Kenya ambao ni Majirani zetu Muungano wa CORD ukiongozwa na Raila Odinga kushinda uchaguzi wa Kenya ambao utakuwa wa amani na utulivu na kuwashinda Kina uhuru Kenyatta na Ruto na Muungano wao wa JUBILEE na ule wa Musalia mudavadi unaoitwa AMANI

Maalim Hassan Yahya Hussein
13/1/2013 Jumapili

No comments:

Post a Comment