Siku ya Jumatano
Jioni Kupitia Mitandao Ya Kijamii Facebook, Twitter na BBM uvumi ulienea kuwa
Mwanamuziki Wa Injili Nchini Tanzania Bahati Bukuku amepoteza maisha. Watu
walikuwa Wakihaha kutafuta ukweli wa habari hizo.
Kama ilivyo ada Ze Blogger alitafuta mawasiliano na Bahati Bukuku ambaye bila
mafanikio namba yake haikupokelewa, ndipo jitihada zikafanyika kuongea na Rais
Wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania Advocate Addo November ambaye
alikanusha juu ya Ukweli wa Jambo hilo. Katika Mazungumzo na Blogger Addo
alisema "Nimesikitishwa sana na kuwepo kwa uzushi huo kutoka kwa Watu,
najua yamkini ni vita tu vya kiroho sababu pia dada yetu anapita sana kipindi
hiki katika battle, yeye ni mzima nimeongea nae na Hatutakufa bali
tutaoshi"Rais Wa Shirikisho alienda Mbali zaidi kwa kuandika katika
Facebook Wall yake.
No comments:
Post a Comment