Mwanamuziki mkongwe kutoka
Tanzania, Profesa Jay
amezushiwa kufariki dunia leo... Habari hizo ambazo zimesambaa mtandaoni ikiwa
ni zaidi katika mitandao ya jamii zikizusha msanii huyu maarufu na wa siku
nyingi kufariki dunia... WHAT???
Hii si mara ya kwanza kwa
watu maarufu nchini Tanzania
kuzushiwa kufa, hivi karibuni msanii AliKiba
pia alizushiwa kufariki dunia kwa ajali ya gari jijini Dar, lakini habari
zikaja kuthibitishwa kuwa si kweli....
Baada ya tuhuma hizi, ambazo hazijaeleweka zilipoanzia, Profesa Jay a.k.a Heavy Weight Mcee
alianza kupokea simu mbalimbali kutoka kwa watu wake wa karibu kutaka
kuhakikisha ni kweli ama la.
Habari hizi zilimshtua yeye
pia na kuamua kuandika kwa watu wake kupitia ukurasa wa twitter kudhihirisha
yuko poa na ni mzima kabisa.
No comments:
Post a Comment