Washukiwa
wa kundi la kiisilamu wamewakata vichwa watu kadhaa mjini Maiduguri, Kaskazini
mwa Nigeria.
Mtu mmoja
ameambia BBC kuwa wanaume watano waliuawa wakati wa msako katika nyumba za watu
usiku wa kuamkia leo.
Miongoni
mwa walionyongwa ni baba na mwanawe.
Hata
hivyo, jeshi la Nigerialimesema ni watu watatu pekee waliouawa.
Zaidi ya
watu 20 sasa wamefariki katika mashambulizi tofauti, Kaskazini mwa Nigeria wiki
hii pekee ambayo yanshukliwa kusababishwa na kundi la
Boko
Haram pamoja na makundi mengine yanayotaka nchi hiyo kutumia sheria za
kiisilamu.
Boko
Haram wamelaumiwa kwa mauaji ya watu 23 katika mashambulizi tofauti Kaskazini
mwa Nigeria.
Walio
shuhudia mauaji hayo wanasema kuwa washambuliaji waliwalenga watu waliokuwa
wanauza nyama ya wanyamapori, katika eneo la Damboa siku ya Jumatatu na kuwaua
watu 18.
Watu
wengine watano walifariki Jumanne wakati kundi la wanaume waliokuwa wanacheza
mchezo wa kamari walishambuliwa mjini Kano.
Kundi la
Boko Haram, linalopigana kutaka kuweka sheria za kiisilamu, nchini Nigeria
limekuwa likifanya mashambulizi, katika sehemu kadhaa nchini humo.
Boko
Haram imelaumiwa kwa vifo vya takriban watu 1,400, Kaskazini mwa Nigeria tangu
mwaka 2010. Mwaka jana pekee , kundi hilo lilihusishwa na vifo vya watu 600.
Siku ya
Jumatatu, watu waliokuwa wamejihami, walifyatulia risasi katika soko moja jimbo
la Borno , wakiwalenga watu waliokuwa wanauza nyama ya nyani, na nguruwe.
Waisilamu
wengi hawatumii kabisa nyama ya wanyama pori.
"watu
waliokuwa wamejihami, na wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram,
walikuja katika soko moja eneo hilo, na kuwapiga risasi watu 13, papo hapo na
wengine watano walifariki kutokana na majereha yao.'' alisema afisaa mmoja.
Eneo la
Damboa liko karibu na hospitali moja mjini Borno katika jimbo la Maiduguri,
ngome ya Boko Haram.Kundi hilo liliundwa mjini humo mwaka 2002.
Wakati
huohuo, ripoti zinasema kuwa shambulizi lengine baya sana limefanywa mjini Kano
, mji mkuu Kaskazini mwa Nigeria,umbali wa kilomita 500, Magharibi mwa Damboa.
Watu
waliokuwa wanaendesha pikipiki waliwanywaftulia risasi, vijana waliokuwa
wanacheza nje , kwa mujibu wa taarifa za polisi.
Mchezo wa
kamari pia umeharamishwa katika dini ya kiisilamu.
No comments:
Post a Comment