Leo hii nilipozungumza na
wafanyakazi wa TTCL. Shirika hili lina changamoto nyingi. Tumezizungumza zote.
Tumedhamiria kuliinua Shirika hili. Wafanyakazi wamenikabidhi kabrasha lenye
tuhuma dhidi ya uongozi. Nimewasiliana na TAKUKURU na kuliwasilisha kabrasha
huko ili uchunguzi ufanyike, na itakapobainika kuna makosa, wahusika wakamatwe
na kupelekwa mahakamani. Bodi pia ina nafasi yake katika kuamua kama utaitishwa
ukaguzi maalum wa CAG. Katika wiki chache zijazo, tutapata uongozi mpya na pia
tunatarijia kuanza mchakato wa kulimiliki Shirika kwa asilimia 100 (kwa sasa
AirTel ina hisa asilimia 35 katika TTCL)
No comments:
Post a Comment