Rais wa zamani wa Misri, Hosni
Mubarak, ameruhusiwa kufanyiwa kesi nyengine kwa makosa ya kutozuwia mauaji ya
waandamanaji mamia kadha wakati wa ghasia zilizomuondoa madarakani.
Mahakama ya rufaa mjini Cairo, baada
ya kikao kifupi, yalitoa amri hiyo ya Bwana Mubarak kufanyiwa kesi nyengine.
Mwezi wa Juni mahakama yalitoa
hukumu ya kifungo cha maisha kwa Rais Mubarak kwa hatia ya kuwa na dhamana ya
mauaji ya waandamanaji yaliyofanywa na askari wa usalama ambao wakijaribu
kuzima ghasia za mwaka wa 2011.
Mkuu wa usalama wa Bwana Mubarak,
Habib el-Adly, ambaye anatumika kifungo cha maisha kwa mashtaka kama hayo, piya
atafanyiwa kesi nyengine.
No comments:
Post a Comment