![]() |
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene. |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza ratiba ya uchaguzi wake wa ndani, inayoonyesha kuwa kitapata mwenyekiti mpya ifikapo Desemba 13, mwaka huu.
Ratiba iliyotolewa na chama hicho Dar es Salaam
jana imeeleza kuwa uchaguzi huo wa mwenyekiti, utatanguliwa na chaguzi
nyingine za ngazi za majimbo, mkoa, wilaya, kata na tawi.
“Uchaguzi utaanza Aprili, mwaka huu na tunatarajia
umalizike Desemba mwaka huu kwa kumchagua mwenyekiti taifa,” alisema
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika.
Alisema kuanzia Aprili hadi Septemba kutafanyika
chaguzi katika ngazi za msingi ambazo zinajumuisha matawi, majimbo na
wilaya kabla uchaguzi huo haujafanyika katika ngazi ya mkoa kuanzia
Novemba.
“Uchaguzi ngazi ya taifa utahusisha pia jumuiya za
chama ambazo ni Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Baraza la Vijana
(Bavicha), Wazee, Kamati Kuu na Baraza Kuu Taifa,” alisema.
Nafasi nyingine zitakazoshindaniwa ni za wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa.
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment