Friday, January 18, 2013

WEMA SEPETU AMALIZA BIFU NA MAMA YAKE


Waswahili hawakukosea kusema ndugu wakigombana shika jembe ukalimeautiani sana na yaliyomtokea mzee yusuph mfalum wa taraaabu na dada yake khadija yusuph pale wanapogombana na mara wanapata sasa kihoja ni hichi hapa

YULE mwanadada mwenye sura ya mauzo katika filamu za Bongo, Wema Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu wamemaliza bifu lao,na sasa ukiwaona ni kama kumbikumbi......

Bifu hilo lilionekana limekwisha wakati wa Arobaini ya mama wa Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema, iliyofanyika nyumbani kwao Kinondoni-Studio, Dar, Wema alibambwa akimfuata mama yake aliyekuwa pembeni na kumkumbatia huku akimdekea.

Mama na mwana hao ndivyo watu walivyosikika . waliendelea kubembelezana na kuwafanya watu waliokuwa eneo hilo kuwashangaa kutokana na kumbukumbu za hivi karibuni ambapo walitofautiana kiasi cha Wema kukataa mama yake asifike kwake.

“Nampenda sana mziwanda wangu huyu, we’ acha tu, japokuwa muda mwingine ananikosea. Unajua napenda kuwa naye muda wote lakini kutokana na majukumu aliyonayo kuonana ni tabu, lakini Wema kwangu bado ataendelea kuwa mtoto siku zote.”

Aidha, wakiwa wanaendelea kupiga stori za hapa na pale, mama huyo alimchombeza bintiye kuhusu kula ice cream
ambapo Wema alidakia na kumwambia mama yake kuwa asijali wakimaliza shughuli za arobaini hiyo watakwenda.

“Usijali mama yangu, tukimaliza hapa tutakwenda. Mimi nipo wala huwezi kukosa kitu ambacho unakitaka,” alisema Wema.

Mwishoni mwa mwaka jana, Wema alimkasirikia mama yake huyo kufuatia kuanika runingani mambo ambayo binti yake hakuyapenda yawe wazi.

Huyo ndio wema asante mama kwakumpenda mwanao.

No comments:

Post a Comment