Mamlaka ya hali ya hewa
ilitoa taarifa juu ya mvua zinazonyesha na kuwataadharisha wale wakaao mabondeni
wananchi waishio maeneo
ya jangawani kata ya mchikichini wanaiomba Serikali iwatengenezewe miundombinu
ya sehemu hiyo ili waendelee kuishi katika maeneo hayo.
"kama serikali
inaweza kutengeneza barabara na sisi watuzibie huo mto lakini kuhama
haitawezekana tutaenda wapi"mmoja wa wakazi hao wa jangwani alisema.
Mjumbewa eneo hilo Bw.
Nurdin Omary aliomba serikali itengeneze mfereji kwa kujengea kuta kwenye kingo
za mto unaopita eneo hilo .
Wakati huohuo kijiji cha
Kunyansulumutu mkoani Mara, mto mara unaopita eneo la wilaya ya serengeti
umefurika na watu wanokaa maeneo ya jirani wanaishi juu ya miti,makazi ya
wanakijiji hicho wameathirika pamoja na mifungo na mazao yao.hali inaonekana
kuwa mbaya sana eneo hilo.
No comments:
Post a Comment