WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa
kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.
“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo
ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe.
, ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na
subira katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna
gesi asilia.
Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi
kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni mali ya Watanzania wote na
siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.
Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano yasiyokuwa na
msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza rasilimali za wananchi bila
faida.
“Salamu zangu za mwaka mpya ni kuwaomba madiwani kuacha kutumia
vikao kuwajadili madiwani wenzenu kwa hoja zisizokuwa na maana, badala yake
tujenge umoja na mshikamano ili kufanya kazi za kusimamia miradi ya maendeleo,”
alisema Membe.
Waziri Membe alitumia muda huo pia kuwataka madiwani kujipanga
katika kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya Halmashauri.
Baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali mikoa
ya Lindi na Mtwara walikusanyika jimboni kwa Membe kusherekea kuadhimisha mwaka
mpya.
Viongozi walioshiriki katika sherehe hiyo ni pamoja Mbunge wa
Mtwara mjini, Hasnain Murji, Godless Kweka ambaye ni Mjumbe wa Nec, wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Ludovick Mwananzila
na madiwani pamoja na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.
Source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment