Ripoti kuhusu hali ya chakula duniani kwa mwaka 2012 iliyotolewa
leo na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa-FAO, imeonyesha kuwepo makadirio
mapya ya hali ya ukosefu wa chakula duniani.
Ripoti hiyo ya mwaka inayosisitiza zaidi juu ya umuhimu wa kuongeza kiwango
cha uwekezaji katika kilimo ili kusaidia kupunguza njaa na umasikini duniani
iliyozinduliwa leo mjini Roma, imeonyesha kwamba mafanikio katika kupunguza
tatizo la njaa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita yameongozeka kuliko
ilivyokuwa ikiaminika hapo kabla. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, huenda malengo ya Maendeleo ya Milenia kuhusu kupunguza njaa na umaskini yatafikiwa ifikapo mwaka 2015, kutokana na makadirio mapya ya lishe kuboreshwa kwa mbinu na mikakati mbalimbali. Mafanikio mengi yalipatikana hasa katika kipindi cha mwaka 2007 na 2008 na tangu wakati huo, mafanikio ya kupunguza njaa yalianza kupungua. Hata hivyo, idadi ya watu wanaokabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa chakula cha kutosha bado iko juu na jitihada za kumaliza tatizo la njaa bado linabakia kuwa changamoto kubwa duniani.
No comments:
Post a Comment