Mtu aliyekuwa na silaha nzito amefanya mashambulizi katika shule ya
awali iliyoko Newtown kwenye jimbo la Connecticut, nchini Marekani na
kuwaua watu 26 wakiwemo watoto wadogo 20 wenye umri kati ya miaka 5 hadi
10.
Mtu huyo anayekadiriwa kuwa katika umri wa miaka 20, alivamia darasa
kwenye shule hiyo ambayo mama yake alikuwa mwalimu na kumfyatulia risasi
mama yake pamoja na wanafunzi 18 darasani humo kabla ya kuwauwa watu
wazima watano na kisha kujiua mwenyewe.Wanafunzi wengine wawili walifariki wakiwa hospitalini kutokana na majeraha waliyopata. Polisi wamesema kuwa hilo ni moja kati ya matukio mabaya ya mauwaji ya raia katika historia ya Marekani. Polisi imesema kuwa mtu huyo alikutwa amekufa ndani ya shule hiyo.
Muuwaji anaripotiwa alikuwa na silaha nne za mkononi na alivalia mavazi ya kujikinga na risasi. Mtu mwingine alikutwa amekufa kwenye mji huo wa Newtown na kufikisha idadi kuwa 28.
No comments:
Post a Comment