Mbunge wa jimbo la
Ubungo, John Mnyika akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo,
Shuka, Godoro na Chandarua pamoja na fedha taslimu kiasi cha sh. laki saba kwa
Makamu Mwenyekiti wa timu ya soka ya Wanawake ya Mburahati Queens, Ridhwan
Mkasa kwa ajili ya kuisaidi timu hiyo.
Na Elizabeth John
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika
(Chadema ) amelitaka Shilikisho la saka Tanzania (TFF) kutoa mchanganuo kwa
dola 250 za Marekani zinazotolewa na Shirikisho la soka Duniani (FIFA) kila
mwaka kwa ajili ya kuendeleza soka nchini.
Mnyika aliyasema hayo jijini Dar es Salaam
jana wakati alipokabidhi msaada wa shilingi milion 1.5 pamoja na godoro moja likijumuishwa kwenye
fedha hizo kwa timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Mburahati Queens.
“TFF inaulazima wa kutoa ufafanuzi kuhusu
fedha hizo ambazo zinatolewa kwaajili ya kukuza soka la vijana na wanawake,
wanatakiwa kuchanganua kwa kiwango ambacho kulitumika kuanzia Juni mwaka jana
hadi Juni mwaka huu na matumizi yaliyoanza kutumika Julai yanatakiwa yaelekeze
ni kiasi gani kimetengwa kwaajili ya vijana na wanawake,” alisema Mnyika.
Mburahati Queens ilipewa msaada huo baada
ya timu hiyo kutembelea bungeni mjini Dodoma kwaajili ya kuhamasisha
upatikanaji wa Katiba mpya.
Mnyika alisema shilingi laki tano
zilichangwa na wabunge viti maalumu na
kukabidhiwa kwake na Waziri kivuli wa Habari Utamaduni na Michezo Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’ katika kikao kilichopita.
Pia baada ya kurudi kutoka bengeni katika
kikao kilichopita Mnyika alikusanya michango mingine kwa wadau wengine na
michezo na hadi kufikia kiwango kicho.
Mnyika aliuomba uongozi wa timu hiyo
kuandaa mchezo mwingine wa kuwahamisisha wananchi wa Jimbo la Ubungo kujitokeza
kutoa maoni yao kwa wajumbe wa tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya.
“Kutokana na Kamati ya Katiba kufika katika
Jimbo letu mnatakiwa kujitahidi kuandaa mchezo wa kirafiki ili kuhamisisha
wananchi kujitokeza katika utoaji wa maoni ya Katiba Mpya,” alisema Mnyika.
No comments:
Post a Comment