Mwili wa mwanamke wa India ambaye amefariki hospitalini nchini Singapore
baada ya kubakwa kinyama mjini New Delhi utarejeshwa kwa ndege maalum
ya kukodi baadaye leo Jumamosi(29.12.2012).
Balozi wa India nchini Singapore T.C.A Raghavan amewaambia
waandishi habari, saa kadha baada ya mwanamke huko kufariki
kutokana na viungo vyake kushindwa kufanya kazi katika hospitali
nchini Singapore ambako alikuwa akipatiwa matibabu.Mwanamke huyo na ndugu wa marehemu watasafirishwa kwenda India katika ndege maalum ya kukodi baadaye mchana wa leo Jumamosi, (29.12.2012) , amesema Raghavan.
No comments:
Post a Comment