Rais wa kwanza wa Afrika Kusini
Nelson Mandela, anayetibiwa kwa ugonjwa wa mapafu, anaendelea vyema na matibabu
yake na kwamba hali yake imeimarika.
Bwana Mandela,mwenye umri wa miaka
94, alikimbizwa katika hospitali ya kijeshi, mjini Pretoria, siku ya Jumamosi.
Madaktari wanaomtibu Mandela
wameelezea kuridhika na anavyopata nafuu. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka
kwa ofisi ya rais Jacob Zuma.
Taarifa za bwana Mandela kuendelea
kuwa hospitalini, zimezua wasiwasi nchini Afrika Kusini.
Magonjwa ya mapafu yanaweza
kusababishwa na virusi au viini tete. Pia yanaweza kusambazwa kupitia kwa
kikohozi au kupiga chafya na yanaweza kuambukizwa kwa kugusa sehemu ambazo
mgonjwa amegusa.
Kuna majina tofauti ya magonjwa
ikizingatiwa sababu na sehemu ya mwili ambapo ugonjwa ule umeambukizwa.
No comments:
Post a Comment