Godbles Lema, amewasilisha sababu 18, kuiomba Mahakama ya Rufaa nchini, itengue hukumu ya awali iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili mwaka huu ambayo ilifuta ubunge wake.
Rufaa hii inatoka na hukumu iliyotolewa jijini Arusha na kumvua Ubunge Bw.Gobless Lema iliyowasilishwa mahakamani na makada wa CCM.Baada ya kusikilizwa kwa hukumu hiyo Bw.Lema amesema wapenzi wake na wanachama wa CHADEMA waamini ushindi na hukumu yeyote itakayotolewa itakuwa ni mpango wa Mungu kwa kuwa mambo yote amemwachia Mungu.
Wakati huohuo wakili wa Bw.Lema ,Tundu Lissu mlisema mpambano ulikuwa mkali na kwa sasa mzigo wameutua kwa Majaji wa Mahaka hiyo ya Rufaa kuamua
No comments:
Post a Comment