Hatima ya ubunge wa Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha
mjini Bw.Godbless Lema itajulikana kesho ambapo majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa itapokaa na kutoa uamuzi
juu ya rufaa hiyo,
Rufaa hiyo itasomwa kesho 21.12.12 saa tatu asubuhi katika
mahama ya rufaa .
Bw.Lema alivuliwa ubunge mnamo April 5 mwaka 2012 katika
hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel
Rwakibalia baada ya kesi iliyofunguliwa na makada 3 wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM),Bw.Musa Mkanga,Bi.Happy Kivuyo na Bi.Agness Mollel wakipinga
ushindi alioupata Bw.Lema katika uchaguzi ulifanyika mwaka 2010
No comments:
Post a Comment