![]() |
MFANO WA TABLET ZA VIM KUTOKA AFRIKA |
Simu aina ya smartphone na kompyuta za tablet zinazosemekana
kuwa vifaa vya mawasiliano vya kwanza kutengenezwa na kampuni ya Afrika
zimezinduliwa.
Vifaa hivyo, ambavyo vimebuniwa na mjasiriamali wa Congo,vinatengenezwa
nchini China.Kampuni yake ya VMK, vifaa vyake vinaendeshwa kwa teknolojia ya Android ya Googles.
Simu hizo za smartphone zitauzwa kwa bei ya rejareja ya dola $170, sawa na pauni za Uingereza (£105) na kompyuta itauzwa kwa dola $300 sawa na pauni (£185).
"Ni Waafrika wenyewe, ndiyo watakaofahamu mahitaji ya Afrika," amesema Bwana Mankou katika mkutano wa Tech4Africa mjini Johannesburg.
"Apple ni kampuni kubwa Marekani, Samsung ni barani Asia na tunataka VMK kuwa kampuni kubwa barani Afrika."
Blogu ya teknolojia ya Smartplanet
imeripoti kuwa kompyuta za VMK zinatoa huduma ya uunganishaji wa wi-fi na uwezo
wa gigabytes 4 ambazo zimehifadhiwa ndani yake.
![]() |
Verone Mankou, ndiye aliyeunda kifaa hiki |
Jina lake, Way-C, lina maana ya
"mwanga wa nyota" katika lugha ya Kilingala.
Simu hiyo ya smartphone nyuma na
mbele ina kamera na skrini ya ukubwa wa inchi 3.5 sawa na sentimita 8.9.
Kuna mipango ya kuuza simu hizi
katika nchi kumi za Afrika Magharibi pamoja na Ubelhiji, Ufaransa na India.
Bwana Mankou amesema anatarajia
kuzindua uuzaji wa kompyuta za bei nafuu zaidi kwa wanafunzi mwaka ujao.
VMK imesisitiza kuwa wakati bidhaa
zake zinatengenezwa China kwa sababu za unafuu wa gharama, ubunifu na uhandisi
wa simu hizo ni wa Kiafrika.
Hii ni kutokana na baadhi ya watu au kampuni za biashara kupinga uwezo wa kampuni hiyo katika teknolojia ya simu na kompyuta.
Hii ni kutokana na baadhi ya watu au kampuni za biashara kupinga uwezo wa kampuni hiyo katika teknolojia ya simu na kompyuta.
Kampuni ya VMK imesema kinyume na
bidhaa nyingine za awali za simu na komputa zilizosemekana kuwa za Afrika,
bidhaa za VMK hazifanani na bidhaa zozote za aina hiyo katika nchi nyingine.
Habari kwa Hisani ya BBC-Swahili
No comments:
Post a Comment