Tuesday, December 18, 2012

MWENDESHA MASHTAKA MKUU AJIUZURU

Mwendesha mashtaka mkuu wa Misri, Talaat Ibrahim amejiuzulu wadhifa huo baada ya kukabiliwa na shinikizo la kumtaka ajiuzulu kutoka kwa majaji na waandamanaji. Wote walikarisirishwa na madai kwamba uteuzi wake mwezi jana uliofanywa na Rais Momahed Mursi ulihujumu uhuru wa mfumo wa mahakama nchini humo. Mursi awali alimfuta kazi mtangulizi wa mwendesha huyo mkuu wa mashtaka, Abdel Maguid Mahmoud. Mahmoud alikuwa amehudumu kwa miaka mingi katika wadhifa huo chini ya rais wa zamani Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani kufuatia vuguvugu la umma la kutaka mageuzi mnamo Februari mwaka wa 2011. Kujiuzulu kwa Ibrahim kunatarajiwa kuwasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Mahakama Jumapili ijayo. Majaji wengi wamelalamika kuhusu amri aliyotangaza Mursi mnamo Novemba 22 iliyomlikimbikizia mamlaka mengi. Hali hiyo ilizusha maandamano ya kitaifa na mapambano makali kati ya wafuasi wa Mursi na wapinzani wake.

No comments:

Post a Comment