Mazungumzo baina ya ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Kongo pamoja na waasi wa kundi la M23 yameanza rasmi mjini Kampala Uganda,
chini ya usuluhishi wa mwenyekiti wa nchi za kanda ya maziwa makuu.
Mazungumzo hayo yataendelea, licha ya mkasa uliotokea jana, baada ya ujumbe
wa waasi kuilaumu serikali ya Kongo kuwa inawafadhili waasi kutoka nchi jirani
na walio tishio kwa usalama wa nchi hizo pamoja na raia wa mashariki mwa Kongo.
No comments:
Post a Comment