Wednesday, December 19, 2012

ZUMA ASHINDA TENA

Rais Jacob Zuma amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa kiongozi wa chama tawala nchini humo cha African National Congress ANC.
Zuma alipata idadi kubwa ya kura zilizopigwa na wajumbe elfu nne wa chama hicho wakati wa mkutano wao uliofanyika Mangaung.
Tangu mwanza wa zoezi hilo, Rais Zuma, alitarajiwa kushinda na idadi kubwa ya kura dhidi ya mpinzani wake wa pekee ambaye pia ni naibu makamu wa rais Kgalema Motlanthe.
Bwana Motlanthe sasa amepoteza nafasi yake ya naibu kiongozi wa chama hicho na mahala pake pamechukuliwa na mfanyabiashara maarufu na mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi Cyril Ramaphosa, ambaye sasa atakuwa makamu wa rais wa Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment