Katiba mpya wa Misri iliyoandikwa na bunge linalodhibitiwa na
Waislamu imepitishwa kwa asilimia 64 katika duru ya pili ya kura ya maoni.
Afisa mmoja wa chama cha Udugu wa kiislamu amefahamisha kuwa katiba mpya ya
Misri imepitishwa na wapiga kura wa nchi hiyo baada ya
kufanyika duru ya pili ya kura ya maoni. Afisa huyo ameyakariri matokeo ya
kura ambayo siyo rasmi ya chama chake.Katika duru ya pili ya kupiga kura iliyofanyika hapo jana watu wa Misri waliipitisha katiba mpya kwa asilimia 64. Katika duru ya kwanza asilimia 57 ya washiriki walipiga kura ya ndio. Afisa huyo aliekuwamo katika chumba kilichofuatilia upigaji kura, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa kwa mujibu wa hesabu za chama chake matokeo kamili ya duru ya pili ni asilimia 71 ya kura za ndio.
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa
Stars imeilaza timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo kwa bao moja kwa bila
katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa katika uwanja wa taifa mjini
Dar es Salaam, Tanzania.
Katika mechi hiyo bao pekee la
washindi, lilipatikana sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza
likitiwa kimiani na mshambuliaji Mrisho Ngassa.
No comments:
Post a Comment