Thursday, December 27, 2012

MLIPUKO WATOKEA LAGOS

Taarifa zinaarifu kuwa moto huo ulianza katika eneo la kuhifadhi baruti na kisha kuenea kwa haraka katika majengo mengine yaliyo karibu na ghala hilo.
Moshi mkubwa umeenea kote katika kisiwa cha Lagos na wazima moto wanajithidi kuuzima moto huo.
Bado baadhi ya majengo yanaendelea kuteketea.
Maafisa wa kuzima moto walikuwa na wakati mgumu kufika eneo hilo kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa hapa.
Kwingineko, maafisa wa usalama Kaskazini mwa Nigeria wanasema watu waliojihami kwa bunduki wamefyetua risasi na kuwaua watu sita katika kijiji chenye idadi kubwa ya wakristo.
washambuliaji hao waliwafyatulia risasi waumini katika kanisa dogo wakati wa ibada ya Krismasi.
Mshambuliaji mmoja amezuiliwa na maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Ripoti zaidi zinasema kuwa ulinzi umeimarishwa ili kuwaondoshea wasiwasi wakaazi wa eneo hilo.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo katika jimbo la Yobe, lakini kundi lenye itikadi kali za dini ya Kiislamu la Boko Haram limekuwa likiwalenga Wakristo katika eneo hilo mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment