Tuesday, December 4, 2012

BASI LATEKWA

Basi lilikuwa likisafiri kuelekea jijini Mwanza,lilitekwa usiku wa kuamkia juzi maeneo ya Igunga mkoani Tabora katika kijiji cha Igogo.
Basi hilo la Muro lilikuwa likielekea jijini Mwanza lilipofika maeneo ya kikiji cha Igogo kilometa 13 kutoka Igunga mjini lilikutana na mawe yakiwa yamepangwa barabarani na kuwazuia wasiendelee na safari na ndipo kundi la watu wanaokadiriwa kufikia 15 walipovamia na kuwaamuru abiria waliokuwamo ndani ya basi hilo kutoa simu na fedha walizokuwa nazo na hatimaye kuwavua nguo.
Abiria 3 walijeruhiwa,wakati huohuo Jeshi la Polisi limejipanga kufanya msako mkali ili kuwakamata waporaji hao

No comments:

Post a Comment