Monday, January 7, 2013

KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TANGU KIFO CHA MH.REGIA MTEMA

Regia Mtema Foundation imeandaa kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Regia itakayofanyika siku ya jumatatu ya tarehe 14 Januari 2013 Peacock Hotel. Kutakuwa na mdahalo utakaoanza saa 9 alasiri na kufuatiwa na hafla ya chakula cha usiku.
kwenye mdahalo kutakuwa na mada zifuatazo;
1. Nafasi ya kijana katika kuleta maendeleo na kuchochea demokrasia itatolewa na         Mh.January Y. Makamba
2. Historia ya Regia ( biography)
3. Mada kuhusu rushwa kutoka kwa TAKUKURU mkoa wa Kinondoni
4. Ulemavu sio kutoweza ( disability is not inability) itatolewa na mwenyekiti CHAWATA Tunawakaribisha sana. Tunaomba yule mwenye kupenda kushiriki aseme kwa maandalizi zaidi

No comments:

Post a Comment