Ngoja niweke wazi kabisa.
Ninaulizwa sana kuhusu suala la Urais 2015 baada ya kauli za wanachama
waandamizi wa CHADEMA kunukuliwa kuzungumzia suala hilo. Jibu langu kwa wote
wenye kutaka kusikia kauli yangu ni kwamba 'katika moja ya maazimio yangu ya
mwaka mpya 2013 ni kutoongelea kabisa suala la Urais 2015. Hivyo sitaongelea
suala hili. Sitasema kitu kuhusu suala hili mpaka baada ya Katiba mpya
kupatikana na chama changu kuweka utaratibu na mchakato wake'
No comments:
Post a Comment